Rais Ruto azindua Baraza lake la Mawaziri
- Marvin Francis
- Sep 27, 2022
- 1 min read

Rais William Ruto amewatambulisha wateule wake wa Baraza la Mawaziri leo. Picha: William Ruto. Chanzo: Facebook
Wiki mbili baada ya kuapishwa kama mkuu wa tano wa taifa la Kenya, Rais William Ruto mnamo Jumanne aliwatambulisha wajumbe wake wa Baraza la Mawaziri.
Kuzinduliwa kwa baraza la mawaziri kulikuja muda mfupi baada ya kufanya kikao chake cha kwanza cha baraza la mawaziri na waliokuwa makatibu wa baraza la mawaziri waliohudumu chini ya Rais wa zamani Uhuru Kenyatta.
Akihutubia taifa kutoka Ikulu ya Nairobi, Rais aliwafungulia Wakenya wanaume na wanawake aliowakabidhi jukumu la kuwasilisha manifesto yake kwa Wakenya.

Makatibu wa Baraza la Mawaziri walioteuliwa hata hivyo watachunguzwa bungeni.
Hii hapa orodha kamili ya wajumbe wake wa Baraza la Mawaziri:
Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri - Musalia Mudavadi
2. Mambo ya Ndani - Kithure Kindiki
3. Hazina ya Kitaifa-Njuguna Ndung'u
4. Utumishi wa Umma na Jinsia - Aisha Jumwa
5. Ulinzi - Aden Duale
6. Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji - Alice Wahome
7. Mambo ya Nje na Diaspora -Alfred Mutua
8. Biashara - Moses Kuria
9. EAC - Rebecca Miano
10. Barabara - Onesmus Kipchumba Murkomen
11. Ardhi - Zacharia Mwangi Njeru
12. Utalii - Peninah Malonza
13. Kilimo - Mithika Linturi1
4. Elimu - Ezekiel Machogu
15. Nishati na Petroli - Davis Chirchir
16. Michezo - Ababu Namwamba
17. Vyama vya Ushirika na MSMEs - Simon Chelugui
18. Madini - Salim Mvurya
19. Kazi - Florence Bore
20. Afya - Susan Wafula
21. Mawasiliano - Eliud Owalo
22. Mazingira na misitu - Roselinda Soipan Tuya
Mwanasheria Mkuu - Justin Muturi
Mshauri wa Usalama wa Taifa - Monica Juma
Katibu wa baraza la mawaziri - Mercy Wanjau
Sina maoni.... Wacha wapambane na serikali yao. Wakitaka hata kuongeza Stevoh simple boyii wafanye hivyo. Hiyo ni yao. #unbotheredatall!
There's nothing you can do to change the list... Let's continue will our normal hustles as we await the country to stabilize.
Sina maoni kwa sabubu hakuna .mama mboga ,n boda,boda huko
What about Sonko and Muthama 😂😂😂😂
Not sure about Defense! I feel it has gone to unfair hands! Kenyan borders need to be safeguarded with high levels of integrity