top of page

MWANAMKE AMUUA MUMEWE, KABLA YA KUJINYONGA-THARAKA-NITHI



Mwanamke mmoja aliripotiwa kumuua mumewe kabla ya kujinyonga katika kijiji cha Kamacuku, Kaunti ya Tharaka Nithi.

Mwili wa Moses Kirimi Mati, mbunifu wa Chuo Kikuu cha Chuka na mkuu wa idara ya mashamba, ulipatikana kwenye dimbwi la damu kwenye maegesho ya nyumba yake Jumatatu asubuhi.


Mwili wa mkewe, Pamela Wanja, uligunduliwa baadaye ukining'inia kwenye balcony ya jengo lao la orofa nne.


Kando ya mwili wa Bw Mati kulikuwa na chuma kilichotapakaa damu kinachoaminika kutumiwa kumpiga kichwani mara kadhaa, na kumpasua fuvu la kichwa.


Nguo za Bi Wanja na gari la kubebea mizigo aina ya Toyota lililoegeshwa karibu na mwili wa Bw Mati pia zilikuwa na madoa ya damu.


Polisi pia waligundua barua ya kujitoa mhanga inayoaminika kuandikwa na Bi Wanja kabla ya kujinyonga na kuomba msamaha kwa watoto wao watatu kwa vifo hivyo.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Maara, Mohamed Jarso alisema mwanamke huyo aliacha barua ya kuomba msamaha kwa watoto wao watatu walio chini ya umri, hata hivyo uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini kiini cha kitendo hicho kiovu.

Kufuatia kukithiri kwa visa vya mauaji katika Kaunti hiyo, Mohamed aliwashauri wanandoa kutafuta njia ya kusuluhisha maswala kwa amani bila kuangamiza maisha.


Miili ya wawili hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Chuka, huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika.

Comments


Subscribe to Our Newsletter

Thanks for submitting!

Donate with PayPal
  • White Facebook Icon

AfricsMedia © 2023. All rights reserved.

bottom of page